English version

Earth from space

Kwa nini kuwa kijani? Kwa nini tunahitaji kuwa na mtindo wa maisha ya kijani? Dunia yetu hii ndo makazi yetu pekee, na itabaki kuwa makazi pekee kwa watoto na wajukuu wa familia zetu na jamii. Tunahitajika kulinda makazi yetu na kuhakikisha ni makazi mazuri kwa ajili yetu sisi kama wanadamu na viumbe vyote hai vinavyoishi.  Soma zaidi…

Emissions from cars, factories, power, airplanes

Matatizo makuu: Matatizo makubwa yanayotukabili kipindi hiki katika mazingira ni kama mabadiliko ya tabia ya nchi, takataka, na kutokomea kwa baadhi ya viumbe haiSoma zaidi…

Cleanup day organised by Nipe Fagio

Unachoweza kufanya: Suluhisho linahusisha kubadlisha mifumo mikubwa, ambayo inayoonekana hatarishi. Bali, mabadiliko makubwa yanaweza kuanza na mabadiliko ya mtu mmoja mmoja. Kila mmoja wetu ana nafasi kutatua haya matatizo kama mwananchi, kama mwanajamii, kama mfanyakazi na katika maisha ya kila siku.. Soma zaidi…

Vegetable seller

Unachokula na kunywa: Hapa Dar es Salaam tumebahatika sana kuwa na machaguo mbalimbali ya vyakula vizuri, vilivyozalishwa nchini, vyenye afya, na vinavyopatikana kipindi chote cha mwaka. Tufurahie! Soma zaidi…

Made in Tanzania tag

Unachokinunua: Nunua vichache, uza na nunua mtumba, nunua vinavyozalishwa nchini, epuka bidhaa za kutumia mara moja. Zingatia uimara wa bidhaa na uwezekano wa kurekebisha kikiharibika. Zingatia nishati na nyezo zilizotumika wakati wa uzalishaji wa bidhaa. Soma zaidi…

Reduce, reuse, recycle

Takataka zako: Je takataka zako ni takataka kweli? Anza kuzitumia kama mbolea zikifaa. Ni rahisi! Punguza matumizi, tumia zaidi ya mara moja na peleka taka kuchakatwa kwa matumizi mengine. Soma zaidi…

Dar es Salaam Cycle Caravan

Usafiri wako: Jinsi unavyosafiri kunaweza kuwa na madhara katika uzalishaji wa hewa ya ukaa. Tembea kwa miguu, kimbia au endesha baiskeli! Kwa safari ndefu, tumia usafiri wa uma! Epuka matumizi ya ndege. Soma zaidi…

Solar water heater

Nyumba na nishati: Hapa Dar, tunaweza kuzingatia ubunifu wa majengo, kuepuka viyoyozi, kupika kwa ufanisi, kutumia nishati ya jua kupashia maji, kutumia umeme wa nishati ya jua, kupunguza matumizi ya vifaa mbalimbali, na kuzingatia ufanisi wa vifaa katika matumizi ya nishati. Soma zaidi…

.

Ungana nasi! Changia mwongozo huu, omba linki, uliza maswali na shea dondoo hizi na wanamazingira wengine Dar. Tuna ukurasa wa facebook unaoitwa Green Dar.

Kurasa ya linki – linki zote sehemu moja

 

Tovuti hii imeundwa na Elaine mwaka 2019. Wasiliana na mimi kwa Mastodon kama utapenda kusaidia kusasisha tovuti hii mastodon.ie/@ElaineActivism . Kama huna akaunti ya Mastodon, unaweza kujiunga hapa mastodon.social